Sunday, January 10, 2010

Togo yajiondoa kwenye michuano ya CAF
















Mchezaji wa Togo Emmanuel Adebayor


Timu ya taifa ya Togo imejiondoa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kufuatia kuuawa kwa dereva wa basi lao.

Wachezaji wawili wa Togo walifyatuliwa risasi na kujeruhiwa katika mkoa wa kaskazini wa Cabinda siku ya ijumaa.

Waandaaji wanasisitiza kuwa michuano itaendelea na kwamba wataimarisha usalama.

Lakini mchezaji wa Togo Alaixys Romao ameliambia gazeti moja la lugha ya kifaransa L'Equipe: "Tunazungumza na timu zengine katika kundi letu kuzishawishi zisusie."

Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.

Ivory Coast na Burkina Faso ni timu zengine zilizopangwa katika kundi B.


Source: BBC