
Sababu zilizotolewa za kunyang'anywa unahodha wa Gallas ni maneno aliyosema Gallas alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na mvutano ndani ya Arsenal.
Nafasi hiyo ya unahodha kwenye pambano la leo inaweza kushikiliwa na kipa Manuel Almunia ama mlinzi Gael Glichy.
Katika mahojiano na vyombo vya habari mwanzoni mwa wiki, Gallas alieleza kuwepo kwa kutokuelewana ndani ya timu katika mechi kadhaa ikiwemo ile ya watani wao wa jadi Tottenham waliotoka nao suluhu 4-4 mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment